Jumapili, 13 Desemba 2015

SIKU TATU ZA MKESHA WA MAOMBI ECWC-MJI WA BWANA


PIA,  UNGANA NASI KATIKA MAOMBI YA KUFUNGA SIKU 21 KUANZIA TAR. 12/12/2015 MPAKA 1/1/2016

MAANDIKO NA MADOKEZO YA MAOMBI YA KUSIMAMIA:
ZABURI 24:1-8
                20:1, 23:1-6, 45: 1-21
1. Mungu asimame kwa ghadhabu yake mwenyewe katika maisha yako
2. Mungu akuongoze kwa yaliyo mema ili uwe sauti ya kuwavuta walio wengi,
3. Bwana asimame na kila shimo lililochimbwa na adui kwa ajili ya walinzi wa Madhabahu
4. Kuziba kila Mifuko iliyotoboka..., ghala zako.
5. Mungu akupe Kibali, neema, hekima, Afya na Maongezeko katika familia, taifa na.........

Jumapili, 1 Novemba 2015





UJUMBE: JINSI YA KUULINDA MUUJIZA WAKO
MNENAJI: ASK. MWAYAHILA

Alianza kwa kueleza vile alivyokuta huduma ambapo anasema, "...sikuamini kuona Ask. Manase akifanya ibada na watoto wadogo... lakini kutokea huko sasa kuna Mji wa Bwana...Nao utaendelea kukua na kupendeza zaidi na zaidi..." hivyo alisisitiza kuwa ni vema muujiza ukatunzwa na ukalindwa kwa uaminifu!

KUMBUKUMBU 28:1

1. SHIKA NENO NA AHADI ZAKE

2. SIKILIZA SAUTI YA MUNGU NA UTENDE YOTE YALIYOANDIKWA KWENYE TORATI.
    ***USIJICHANGANYE NA MAMBO YA DUNIA: UWE MWAMINIFU KWA MUNGU
    (kutoka 15:26)

3. WEKA AHADI NA MUNGU NA UWE MWAMINIFU
     Zaburi 126:5 "wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha"


Alhamisi, 29 Oktoba 2015

UFUMBUZI WA FUMBO LA TATIZO (SIKU YA PILI YA SEMINA YA WEMA NA NEEMA YA MUNGU MARADUFU)



SOMO: UFUMBUZI WA FUMBO LA TATIZO KWA JIBU LA FUMBO

UFUNUO 17:5
DANIELI 2: 22
1 SAMWELI 21: 1
1 SAMWELI 22:21-22
YOHANA 3:8

KARIBU KUJIFUNZA MENGI ZAIDI

UKITAKA CDs ZA MAHUBIRI YA SEMINA HII ZINAPATIKANA KWA KUWASILIANA NASI.

Jumatano, 28 Oktoba 2015

KARIBU KWENYE SEMINA YA WEMA WA MUNGU NA NEEMA MARADUFU HAPA ECWC-MJI WA BWANA: 28/10 - 01/11/2015. NA JUMAPILI YA TAREHE 1/11/2015 TUTAKUWA NA SHEREHE YA ECWC - MJI WA BWANA KUTIMIZA MIAKA MIWILI.



ISAYA 54:1-10
YEREMIA 3:3
2NYAKATI 13:3 (Agano la Chumvi)

FUNGUO ZA KUUPATA WEMA WA MUNGU:
1. TAFUTA MTU SAHIHI
     - watu wengi hawaupati wema wa Mungu kwa sababu wanaambatana na watu wasio sahihi katika           maisha yao... Yusufu alikataa kuambatana na mke wa Potifa ndio maana wema wa Mungu ukawa naye maisha yake yote...
     -ukiambatana na muovu utakuwa muovu na utapishana na wema wa mungu
     -ukiambatana na waaminifu mbele za Mungu nawe utakuwa mwaminifu na hivyo mataifa watakutumikia (Wema wa Mungu); watapamabana kwa ajiri yako nawe utakaa kimya.

     -DAUDI kwa uaminifu alipamabana na dubu na simba waliotaka kuua mifugo ya baba yake; hatima yake ilikuwa kuupata wema wa Mungu.
     -Familia yako, Jamii ya Watanzania inahitaji watu waaminifu. Mahali pasipo na waaminifu hakuna Amani.

2. CHOCHEA UWEPO WA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO
     -Haruni alipata kuwa kiongozi kwa wema wa Mungu na wala hakukuwa na maswali juu ya kwa nini ameteuliwa kuwa kiongozi!!!
     -Mungu huwapenda wale wenye moyo wa kumwabudu yeye: katika kumwabudu hakuna kupungukiwa na chochote.
    - Mwanamke mfoenike aliupata wema wa Mungu kwa kumwabudu Yesu... alisema, "...hata mbwa anastahili makombo..."
    -Wengine wanapishana na wema wa Mungu kwa sababu ya kutotaka kutoa Muda wao kwa Mungu kumwabudu.

3. KUBAKI KUJIFUNGAMANISHA NA WATUMISHI WA MUNGU WA KWELI
    -"...walikombolewa na mkono wa nabii..."

KUJIFUNZA MENGI ZAIDI; KARIBU KWENYE SEMINA ECWC - MJI WA BWANA MBEZI KWA MSUGURI.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...