Jumamosi, 30 Novemba 2013

KONGAMANO LA KANISA LA ELIM PENTEKOSTE TANZANIA, JIMBO LA PWANI LILILOFANYIKA CHALINZE KUANZIA 25-29/11/2013.

WATU WAKIMSIFU YESU KRISTO WAKICHEZA NA KUIMBA NYIMBO ZA SIFA 


MCHUNGAJI TAJU NA MTAFRI WAKE PAUL, WAMISHENARI KUTOKA KAMERUNI WAKIFUNDISHA KUHUSU NGUVU ILIYOPO KATIKA KUMSIFU MUNGU.


KWAYA YA MZEITUNI WA MADHABAHUNI KUTOKA ECWC - MJI WA BWANA MBEZI KWA MSUGULI, DAR ES SALAAM WAKIMUIMBIA MUNGU. 


MAMA ASK. MANASE, D.M., AMBAYE PIA NDIYE MWALIMU WA KWAYA YA MZEITUNI WA MADHABAHUNI AKIMWIMBIA MUNGU. 


MCHUNGAJI EMMANUEL, MMISHENARI KUTOKA KAMERUNI AKIFUNDISHA KWA MFANO KUHUSU UTHAMANI ALIYONAO MWANA WA MUNGU AKIWA DUNIANI.

Jumamosi, 31 Agosti 2013

NI SIKU YA PILI TANGU KUANZA KWA KONGAMANO LA WANAWAKE WA KANISA LA ELIM PENTEKOSTE TANZANIA (KEPT) JIMBO LA MASHARIKI NA PWANI. HUKU MAMBO NI FURAHA NA KUJIFUNZA MENGI. KARIBUNI SANA!!

Mrs. Magreth Washira akifundisha athari za kuzungumza pasipo sababu za msingi katika jamii/familia. aliwafundisha kwa kutumia mfano wa kunywa maji kujizuia kuzungumza yasiyolazima ili kuokoa ndoa za watu wengi zinazovunjika kwa kuzungumza sana.


sifa zikavuma na wachungaji hawakuweza kuketi, wakasimama kama wanavyoonekana hapo juu wakimchezea na kumwimbia Mungu.


wamama wachungaji wakiongoza kipindi cha kusifu na kuabudu nyakati za jioni.


wamama wachungaji wakiongoza kipindi cha kusifu na kuabudu nyakati za jioni.


wamama wachungaji wakiongoza kipindi cha kusifu na kuabudu nyakati za jioni.


wamama wachungaji wakiongoza kipindi cha kusifu na kuabudu nyakati za jioni. Hapa sifa ikapendeza, kila mtu alicheza namna Roho wa Mungu alivyomuongoza. ilikuwa raha sana kuona watumishi wa Mungu hawa wakimtukuza Mungu namna hii.


kutoka kulia ni Mwimbaji wa Sifa na Kuabu (Mhuville Humphrey) na Mwenyekiti wa Wanawake Tanzania, KEPT (Sifa Mgweno)


Waimbaji wa sifa na Kuabudu (kutoka kulia ni Tito Mgweno na Mhuville Humphrey)


sifa ikazidi kuwa nzuri maana hata watoto nao hawakuona sababu ya kuketi wakati wazazi wao wanamsifu Mungu aletae Furaha na Amani katikati ya kusanyiko hilo.


Askofu wa Jimbo la Mashariki na Pwani, Askofu Manase, D.M akiwa na mke wake wakimsifu Mungu.






Mchungaji Tito Tunda akifundisha kuhusu umuhimu wa kulifahamu neno la Mungu kufanikiwa kiroho na kimwili.

Ijumaa, 30 Agosti 2013

UJENZI WA MJI WA BWANA ENEO LA MBEZI KWA MSUGURU WASONGA MBELE KWA MSAADA WA MUNGU

MJI WA BWANA. Hatimaye ujenzi wa mji wa Bwana eneo la Mbezi kwa Msuguri umeanza kwa kasi. Wiki mbili zilizopita zoezi lilianza kwa Katapila kusafisha eneo na kuwekwa levo sawa. Kwa ajili ya upimaji ili kuruhusu hatua za awali za ujenzi kuanza.
Pichani kwa mbali ni wazee wa kanisa Mzee Tito Mgweno na Mama Roshe Mshanga wakiwajibika kikamilifu katika ujenzi aw maji wa Bwana huko Mbezi kwa msuguri Hakika ilikuwa ni njema na ya kupendeza sana. Tunasema Mungu na awabariki kwa kazi yao njema.
UJENZI WA MJI WA BWANA . Kutokea mahali hapa Kama inavyoonekana pichani ndipo mahali ambapo Madhabahu ya Bwana itakapo simama na kwa hapo wengi watapokea uponyaji, wengi watafunguliwa. ,wengi watabarikiwa, wengi watainuliwa. Shime Watu wa Mungu
UJENZI WA MJI WA BWANA. : Pichani ni Askofu Manasse akipata maelekezo ya hatua za awali za ujenzi wa mji wa Bwana toka kwa Mzee kiongozi wa ECWC Mzee Tito Mgweno ambaye amekuwa akishirikana kwa karibu na kamati ya Ujenzi.

MUNGU AWEZA KUFUNGUA VIFUNGO VYAKO. HII NI IBADA YA JUMAPILI 25.08.2013



Haijalishi umekuwa katika vifungo vya mateso kwa Muda gani lakini Bwana anasema baada ya hayo yote yakupatayo Ni LAZIMA ITENDEKE KWAKO

SUNDAY SCHOOL Ni baadhi ya watoto wa shule ya Jumapili ECWC Ilala Bungoni wakisema mistari ya Biblia waliyojifunza kwa kuikariri ( Aja kwa Moyo) ilikuwa ni ya kupendeza kuona watoto wakilijuwa Neno la Mungu katika umri huu mdogo

MKUTANO MKUBWA WA INJILI TANZANIA KUANZA RASMI 21.08.2013



TANZANIA KWA YESU!!!! Hayawi hayawi sasa yamekuwa lile kusanyiko kuu la Mkutano mkubwa wa Injili kwa mwaka 2013 hapa Tanzania sasa utaanza rasmi siku ya jumatano tarehe 21/8/2013 katakana viwanja vilivyo jirani na uwanja mkuu wa Taifa.

TANZANIA KWA YESU. Pichani ni wanakikundi cha maombi kwa ajili ya mkutano huo mkubwa wakifanya maombi na kuuweka wakfu uwanja utakotumika kwa ajili ya mkutano.

TANZANIA KWA YESU. Pichani ni watumishi wa Mungu toka makanisa mbalimbali wakiwa na viongozi wa Zone zao wakipeana maelekezo na mikakati ili kuhakikisha wanawahudumia Watu watakaofika kwenye mkutano. Hakika ni maumivu makali kwa shetani


YESU AUNGURUMA Ule Mkutano mkubwa wa Injili umeanza kwa kishindo siku ya leo alhamisi kama Inavyoonekana pichani kwaumati mkubwa wa watu kujitokeka kusikiliza neon la Mungu.

Alhamisi, 29 Agosti 2013

KONGAMANO LA WANAWAKE JIMBO LA MASHARIKI NA PWANI 28-31/08/2013 CHALINZE, MKOA WA PWANI. THEME: ENEMY KINGS AND THEIR ARMIES FLEE WHILE WOMEN DIVIDE THE PLUNDER. PSALMS 68:12

Mrs. Margreth Washira kutoka Nairobi, Kenya na Mwl. Sauna Joshua kutoka Morogoro (Wahubiri)

Katibu wa jimbo KEPT, Rev. Jarome Andrea

 Askofu Manase, D.M. akiwaombea watu wakati wa ibada ya Revival.

Mama Gwasa akieleza kuhusu ujasilia mali.

 Washiriki wa kongamano wakisikiliza neno la Mungu wakati wa ibada ya Revival

 kutoka kulia ni Mama Letiva akisoma neno la Mungu wakati Mwl. Sauna akifundisha kuhusu mwanamke na uchumi

kutoka kushoto ni Mch. Tito Tunda (Mujumbe wa Halmashauri Kuu, KEPT) na Mch. Jarome (Katibu, KEPT)
kutoka kushoto ni Askofu Manase, D.M., Mama Askofu Manase, Mama Askofu Mgweno na mwenyekiti wa wamama Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania.
Mwl. Saunna Joshua akifundisha somo la Mwanamke na Uchumi.  

MWANAMKE NA UCHUMI
-pambana kuuondoa ujinga.
-ujinga hauondoki kwa kunena kwa lugha au maombi ila ni kwa kutafuta maarifa.
-penda kujifunza na kuchukua hatua. Usiogope kumuomba anayejua jambo zuri akufundishe.
-tumia wakati vizuri/komboa wakati
Mithali 28/20
 -uwe mwaminifu katika kazi ya mikono yako. Usiwe muongo...











































Mama Askofu Secilia Mgweno akifundisha kuhusu Ufahamu wa Kiroho
Viongozi wa wamama kanisa la Elim Pentekoste jimbo la Mashariki na Pwani (kutoka kushoto ni mwenyekiti, katibu na mtunza hazina)
Askofu Manase, D.M. akifungua kongamano la wanawake jimbo la Mashariki na Pwani.


TUTATEKA NYARA
-mwanamke ndiye anayejenga.
-wanawake wanakwenda kujenga mara baada ya kujengwa kiufahamu wa kiroho kutokea katika kongamano hili.
-maisha ya mtu sio kule anakotoka ila anakokwenda...
-MATH 20/20
-wanawake wengi huwa na shauku na maisha yajayo kuliko baba. Mf. Baba anaweza kupata mshahara na kuumalizia kilabuni lakini mama atafikiri sana  kuhusu mahitaji ya familia. Hivyo, hitaji kubwa la mama ni watoto wake waishi salama katika siku zijazo…kwa hili mlilolifanya ni kujenga kizazi kijacho kufanikiwa kiroho na kimwili katika jina la YESU.
2timotheo 1/5…nikikumbuka imani uliyonayo, tena isiyo na unafiki…
(unakaribishwa sana katika kongamano hili. utajifunza mengi ya kukusaidia wewe, familia yako na vizazi vijavyo kwa utukufu wa jina la YESU) 

THEME: ENEMY KINGS AND THEIR ARMIES FLEE WHILE WOMEN DIVIDE THE PLUNDER. PSALMS 68:12
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...