Jumatano, 31 Julai 2013

IBADA YA KUBARIKI WATOTO SIKU YA JUMAPILI 28.07.2013

   Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Elim Pentekoste Tanzania Askofu Mwayahila akiongoza ibada ya kubariki watoto siku ya jumapili 28/07/2013 kanisani ECWC Ilala Bungoni.


Askofu Manase wa kanisa la Elim Pentekoste Ilala Bungoni akiongoza ubatizo wa maji mengi uliofanyika katika kanisa la FPCT Ilala Mchikichini.
Baadhi ya waumini walioshuhudia ubatizo uliofana sana siku ya jumapili ya tarehe 28/07/2013
Askofu Manase akiomba baraka na kuvunja nira za shetani kwa mmoja wa waliobatizwa siku hiyo.
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Anania Mwasomola akisema neno la shukurani kwa Askofu Manase baada ya kuhudumu kwa njia ya uimbaji siku ya jumapili 28/07/2013 kanisani ECWC Ilala Bungoni
Ilikuwa ni siku ya Baraka kwa dada huyu wa ECWC ambaye alitimiza haki yote siku ya jumapili 28/07/2013
Hakika Roho wa Mungu alihudumia watu walobatizawa siku hiyo. Maana unapomkiri Yesu Kristo na Kubatizwa unafanyika Baraka kwa Mungu maana unavikwa utu upya.
Askofu Manase akiomba baraka kwa damu ya Yesu Kristo ikamfunike dada huyu aliyebatizwa.


Askofu Manase na mama Manase walingoza waumini wengine katika siku ya kubariki watoto kanisani ECWC jumapili ya 28/7/2013 Kama wanavyooneka pichani.

Askofu Mwayahila alisoma neno la Mungu kutoka kitabu cha Yohana sura ile ya 17 ambayo inazungumzia kuhusu kanisa kukaa katika umoja.

Waimbaji wa kwaya ya Mzaituni wa madhabahuni nao walikuwepo katika Ibada ya 28/07/2013 wakimsifu Bwana Kama wanavyooneka pichani.

Waimbaji mbalimbali walikuwepo Kama inavyoonekana pichani Mwimbaji wa nyimbo za Injili Agnes Robert naye akimsifu Mungu kwa njia ya uimbaji.

Mwimbaji Anania Mwasomola akimsifu Bwana kwa wimbo maarufu unaojulikana Kama " wewe ni Baba" Hakika ilikuwa ni siku ya Baraka.


SEMINA YA REHOBOTH YAFANA SIKU YA IJUMAA 27 - JUMAPILI 30/07/201330




Askofu Manase alifundisha na kusema Bwana amemaanisha kukupatia wewe NAFASI , haijalishi itakuwa kwa njia gani lakini ni LAZIMA Bwana akupatie NAFASI. Bwana anasema ni LAZIMA watesi Wako waondoke kwenye njia yako. Na hapo ndipo watakapoulizana ni nani huyo aliyektendea haya.


Askofu Manase alifundisha na kusema Bwana anapokufanyia NAFASI anakomesha vita iliyodhidi yako. Bwana alimwambia Ibrahimu amtoe Isaka kama sadaka.Kwa utayari wa  Ibrahimu ndipo hapo Mungu alivyomfanyia NAFASI kwa kumwambia geuka na mara akamuona kondoo aliyetayarishwa na Bwana mwenyewe, na vivyo hivyo Bwana atakufanyia mlango wa kutokea katika kazi yako, biashara yako na familia yako



Askofu Manase akihubiri Leo katika semina ya siku tatu iliyoanza leo ijumaa katika kanisa la ECWC Ilala Bungoni.Alisema ni wakati wa Bwana kuwafanyia Watu wake NAFASI wakati dunia inawayawaya.Mwanzo 26:12 - 23..... Akakiita Jina lake Rehoboth akasema kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia NAFASI, nasi tutazidi katika nchi



Jumatano, 24 Julai 2013

ASKOFU MANASE BM KATIKA IBADA YA JUMAPILI 21.07.2013 YA KUJAZWA UPYA NGUVU ZA MUNGU KATIKA KANISA LA ECWC



Askofu Manase akimkaribisha Mch Mama Cecilia Mgweno kwa ajili ya Neno la Mungu katika Ibada ya jumapili 21/7/2013 kanisani ECWC.
Waumini wakiwa katika kipindi cha maombi , Hakika Roho mtakatifu aliwahudumia Watu.


Mch Mama Cecilia Mgweno akihubiri , alisema " iko nguvu itendayo kazi ndani yetu nayo ni nguvu ya Mungu "



Waumini wakisiliza neno la Mungu






Mch Mama Cecilia Mgweno alipohubiri alisema " zako nguvu za aina tatu iko nguvu ya kibinadamu, iko nguvu ya shetani na iko nguvu ya Mungu ambayo yapita akili zetu na fahamu kuitambuai."



Sunday School



















Jumatano, 17 Julai 2013

ASKOFU MANASE AHUBIRI UJUMBE USEMAO "BWANA ANATAWALA" SIKU YA JUMAPILI 14.07.2013 KATIKA KANISA LA ECWC

KIPINDI CHA NENO LA MUNGU
Askofu Manase aliweza kuhubiri Neno la Mungu siku hii ya Jumapili

 
 








KIPINDI CHA SHUHUDA


Ndugu Ibrahim Ezekiel akishudia matendo makuu ya Mungu aliyomtendea


KIPINDI CHA SIFA NA KUABUD






KIPINDI CHA SUNDAY SCHOOL






Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...