Jumatano, 31 Julai 2013

IBADA YA KUBARIKI WATOTO SIKU YA JUMAPILI 28.07.2013

   Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Elim Pentekoste Tanzania Askofu Mwayahila akiongoza ibada ya kubariki watoto siku ya jumapili 28/07/2013 kanisani ECWC Ilala Bungoni.


Askofu Manase wa kanisa la Elim Pentekoste Ilala Bungoni akiongoza ubatizo wa maji mengi uliofanyika katika kanisa la FPCT Ilala Mchikichini.
Baadhi ya waumini walioshuhudia ubatizo uliofana sana siku ya jumapili ya tarehe 28/07/2013
Askofu Manase akiomba baraka na kuvunja nira za shetani kwa mmoja wa waliobatizwa siku hiyo.
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Anania Mwasomola akisema neno la shukurani kwa Askofu Manase baada ya kuhudumu kwa njia ya uimbaji siku ya jumapili 28/07/2013 kanisani ECWC Ilala Bungoni
Ilikuwa ni siku ya Baraka kwa dada huyu wa ECWC ambaye alitimiza haki yote siku ya jumapili 28/07/2013
Hakika Roho wa Mungu alihudumia watu walobatizawa siku hiyo. Maana unapomkiri Yesu Kristo na Kubatizwa unafanyika Baraka kwa Mungu maana unavikwa utu upya.
Askofu Manase akiomba baraka kwa damu ya Yesu Kristo ikamfunike dada huyu aliyebatizwa.


Askofu Manase na mama Manase walingoza waumini wengine katika siku ya kubariki watoto kanisani ECWC jumapili ya 28/7/2013 Kama wanavyooneka pichani.

Askofu Mwayahila alisoma neno la Mungu kutoka kitabu cha Yohana sura ile ya 17 ambayo inazungumzia kuhusu kanisa kukaa katika umoja.

Waimbaji wa kwaya ya Mzaituni wa madhabahuni nao walikuwepo katika Ibada ya 28/07/2013 wakimsifu Bwana Kama wanavyooneka pichani.

Waimbaji mbalimbali walikuwepo Kama inavyoonekana pichani Mwimbaji wa nyimbo za Injili Agnes Robert naye akimsifu Mungu kwa njia ya uimbaji.

Mwimbaji Anania Mwasomola akimsifu Bwana kwa wimbo maarufu unaojulikana Kama " wewe ni Baba" Hakika ilikuwa ni siku ya Baraka.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...