Ijumaa, 30 Agosti 2013

UJENZI WA MJI WA BWANA ENEO LA MBEZI KWA MSUGURU WASONGA MBELE KWA MSAADA WA MUNGU

MJI WA BWANA. Hatimaye ujenzi wa mji wa Bwana eneo la Mbezi kwa Msuguri umeanza kwa kasi. Wiki mbili zilizopita zoezi lilianza kwa Katapila kusafisha eneo na kuwekwa levo sawa. Kwa ajili ya upimaji ili kuruhusu hatua za awali za ujenzi kuanza.
Pichani kwa mbali ni wazee wa kanisa Mzee Tito Mgweno na Mama Roshe Mshanga wakiwajibika kikamilifu katika ujenzi aw maji wa Bwana huko Mbezi kwa msuguri Hakika ilikuwa ni njema na ya kupendeza sana. Tunasema Mungu na awabariki kwa kazi yao njema.
UJENZI WA MJI WA BWANA . Kutokea mahali hapa Kama inavyoonekana pichani ndipo mahali ambapo Madhabahu ya Bwana itakapo simama na kwa hapo wengi watapokea uponyaji, wengi watafunguliwa. ,wengi watabarikiwa, wengi watainuliwa. Shime Watu wa Mungu
UJENZI WA MJI WA BWANA. : Pichani ni Askofu Manasse akipata maelekezo ya hatua za awali za ujenzi wa mji wa Bwana toka kwa Mzee kiongozi wa ECWC Mzee Tito Mgweno ambaye amekuwa akishirikana kwa karibu na kamati ya Ujenzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...